Katika kuhakikisha jamii ya wafugaji wa wilaya ya handeni wanainuka kiuchumi halmashauri ya wilaya ya handeni imefungua mnada wa mifugo katika mji wa mkata ambao ulifungwa kwa takribani miaka mitano iliyopita kutokana na mzabuni aliyekuwa akisimamia mnada huo kushindwa kuuendesha kutokana na kukiuka makubaliano ambayo walijiwekea. Akizungumza wakati wa ufunguzi huo mkuu wa wilaya ya handeni GODWIN GONDWE amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuweka usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa ushuru na kuwajuza wafanyabiashara na wafugaji ni kiasi gani kinachotakiwa kulipwa ili kuepusha wafanyabiashara kudhulumiwa na baadhi ya watu.