DC MURO 'Alivyomsweka' Ndani Diwani wa Chadema! Mkuu wa wilaya ya Meru, Jerry Muro, Ameagiza polisi kumkamata Diwani wa Kata ya Maroroni, Edina Mbise. Ndugu Muro amefikia uamuzi huo baada ya Diwani huyo kuchukua mchango wa mifuko 41 ya Saruji kutoka kwa mdau mmoja wa maendeleo iliyokuwa na malengo ya kuchangia ujenzi wa madarasa ya sekondari katika wilaya ya Meru. Diwani Edina Mbise ambaye ni Diwani wa viti maalum wa kata ya Maroroni akiwa ndani ya ofisi za mkuu wa wilaya alikiri kupokea mifuko hiyo wiki moja iliyopita na hakuweza kuifikisha katika shule iliyochangiwa kutokana na kukosa usafiri. Utetezi huo haukueleweka kwa DC Muro ambaye ameagiza askari wamkamate diwani huyo na apelekwe kituo cha polisi ili akatoe maelezo na kisha kwenda kukabidhi Mifuko hiyo ya Saruji. DC Muro ametoa onyo kwa Viongozi wengine kutoshiriki katika vitendo hivyo vya kuhujumu uchangiaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya hiyo kwa kuwa akiwabaini atawashughulikia. #DCMURO Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitte www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jDyho USIKUBALI KUPITWA NA HII, BONYEZA LINK https://www.youtube.com/watch?v=L4UGw. Jiunge na Familia ya Global TV Upande Mtandao wa Mafanikio Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club https://goo.gl/mkvuoB

DC MERUJERRY MUROMKUU WA WILAYA YA ARUMERUDIWANI KATA YA MARORONIEDINA MBISEDC MURO 'Alivyomsweka' Ndani Diwani wa Chadema!MOTO WA DC MURODIWANI WA CHADEMA MARORONIGLOBAL TV ONLINE