Katika kuhakikisha wilaya ya handeni inafanya vizuri katika kilimo na ufugaji wataalamu wa wilaya hiyo yenye halmashauri mbili ya handeni mji na handeni vijijini wamekutana kwa lengo la kutathimini ni kwakiasi gani wameweza kufikia malengo waliyojiwekea kwa miaka miwili iliyopita kuanzia mwaka 2016 mpaka 2018 katika kukuza sekta za kilimo na ufugaji. Wakizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutani huo wataalamu hao wamesema wamefanya vizuri katika mazao ya kimkakati waliyojiwekea hivyo mkusanyiko huo utasaidia kupeana changamoto mbalimbali walizokutana nazo katika utekelezaji wa mikakati yao na baadaye kupatia ufumbuzi wa changamoto zao